Translate

Showing posts with label WATAKATIFU. Show all posts
Showing posts with label WATAKATIFU. Show all posts

Saturday, 7 October 2017

Mtakatifu Karoli Lwanga

Mtakatifu Karoli Lwanga

Mtakatifu-KarolI-Lwanga.jpg


Karoli Lwanga
Karolo Lwanga ndiye maarufu zaidi kati ya wafiadini wa Uganda waliouawa kwa amri ya kabaka Mwanga II (dhuluma za miaka 1885 - 1887).

Pamoja na wenzake anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Wote pamoja walitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa wenye heri tarehe 6 Juni 1920, halafu na Papa Paulo VI kuwa watakatifu tarehe 8 Oktoba 1964
Share:

Mtakatifu Getrudi Mkuu

Mtakatifu Getrudi Mkuu

Mtakatifu-Getrudi-Mkuu.JPG



Mtakatifu Getrudi Mkuu
Mtakatifu Gertrudi (au Getrudi Mkuu) wa monasteri ya Helfta (1256 – 17 Novemba 1301) alikuwa mmonaki wa kike nchini Ujerumani.

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu kama bikira. Sikukuu yake ni 16 Novemba.
Share:

Mtakatifu Fransisko wa Asizi

Mtakatifu Fransisko wa Asizi

Mtakatifu-Fransisko-wa-Asizi.jpg



Mtakatifu Fransisko wa Asizi
Fransisko wa Asizi (kwa Kiitalia Francesco d'Assisi; tangu utotoni jina la ubatizo Giovanni (Battista), yaani Yohane, liliachwa kutumika; pia ubini mwana wa Petro Bernardone ulikuja kuachwa baada ya wao kushindana) alikuwa mtawa, shemasi na mhubiri wa Kanisa Katoliki.

Alizaliwa mwaka 1181 au 1182 mjini Assisi, Italia; alifariki tarehe 3 Oktoba 1226 karibu na mji ule.

Anakumbukwa kwa mtindo wa maisha alipolenga kuiga mfano wa Yesu kila siku.

Alianzisha jumuiya ya kitawa yenye matawi mbalimbali ambayo leo ni utawa wenye wafuasi wengi kuliko yote wakikadiriwa kukaribia milioni moja duniani kote.

Kwa Wakatoliki ni msimamizi wa wanaoshughulikia hifadhi ya mazingira.

Alitangazwa na Papa Gregori IX kuwa mtakatifu tarehe 16 Julai 1228.


Anaheshimiwa na wengi hata nje ya Kanisa lake.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 4 Oktoba.
Share:

Mtakatifu Jorome

Mtakatifu Jorome

Mtakatifu-Jorome.jpg
MT.JOROME
Jeromu au Yeronimo (Strido, leo nchini Korasya 347 - Bethlehemu, Israeli, 420) alikuwa mmonaki, padri na mtaalamu wa Biblia, aliyemudu vizuri lugha zote za kitabu hicho pamoja na Kilatini hata akawa mwandishi bora wa lugha hiyo kati ya mababu wa Kanisa.

Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Mwaka 1298 Papa Bonifasi VIII alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 30 Septemba
Share:

Mtakatifu Maria Gorethi


MTAKATIFU MARIA GORETHI

Maria Teresa Goretti (Corinaldo, Ancona, Italia, 16 Oktoba 1890 - Nettuno 6 Julai 1902) alikuwa bikira ambaye alikataa mfululizo kuzini na jirani yake Alessandro Serenelli, mpaka huyo akamchoma mara 14 mfululizo kwa kifaa cha chuma.

Akizidi kuchomwa, Maria alisisitiza msimamo wake: "Usifanye, ni dhambi!"

Kabla hajafa hospitalini, Maria alimsamehe muuaji wake kwa kumtakia awe naye mbinguni.

Baada ya miaka mitatu gerezani, Alessandro aliongoka na alipotoka alikwenda kuomba msamaha wa mama wa Maria, akakubaliwa kwa hoja kwamba, "Mwanangu amekusamehe wakati wa kufa, nami siwezi kufanya tofauti". Kesho yake walipokea ekaristi pamoja.

Halafu akaishi utawani kwa Wakapuchini wa Macerata hadi alipofariki mwaka 1970.

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 27 Aprili 1947 na kuwa mtakatifu tarehe 24 Juni 1950, wakihudhuria mama yake na muuaji vilevile.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 6 Julai ya kila mwaka.
Share:
Copyright ©| MKATOLIKI KIGANJANI ||CONTACT US 0757195712 ||KILIMANJARO SKY TECHNOLOGIES| |JEMA SOFTWARE DEVELOPER |JEROME MASSAWE||EMMANUEL MALLYA