MTAKATIFU MARIA GORETHI
Maria Teresa Goretti (Corinaldo, Ancona, Italia, 16 Oktoba 1890 - Nettuno 6 Julai 1902) alikuwa bikira ambaye alikataa mfululizo kuzini na jirani yake Alessandro Serenelli, mpaka huyo akamchoma mara 14 mfululizo kwa kifaa cha chuma.
Akizidi kuchomwa, Maria alisisitiza msimamo wake: "Usifanye, ni dhambi!"
Kabla hajafa hospitalini, Maria alimsamehe muuaji wake kwa kumtakia awe naye mbinguni.
Baada ya miaka mitatu gerezani, Alessandro aliongoka na alipotoka alikwenda kuomba msamaha wa mama wa Maria, akakubaliwa kwa hoja kwamba, "Mwanangu amekusamehe wakati wa kufa, nami siwezi kufanya tofauti". Kesho yake walipokea ekaristi pamoja.
Halafu akaishi utawani kwa Wakapuchini wa Macerata hadi alipofariki mwaka 1970.
Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 27 Aprili 1947 na kuwa mtakatifu tarehe 24 Juni 1950, wakihudhuria mama yake na muuaji vilevile.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 6 Julai ya kila mwaka.
0 maoni:
Post a Comment