Translate

Tuesday, 7 August 2018

NOVENA YA AJABU

Image result for novena  ya mtakatifu rita
NOVENA YA AJABU 
Mara upatapo nakala hii, sema sala ifuatayo kwa dhati kwa muda wa siku TISA mfululizo bila kukatiza; Baba yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa Duniani kama Mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu kama na sisi tunavyo wasamehe waliotukosea, usitutie majaribuni lakini utuokoe na yule mwovu, kwa maana ufalme ni wako na nguvu na utukufu hata milele yote, Amina. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele amina. Bikira Maria mama mwenye heri na Neema uniombee kwa Mwanao Bwana wetu Yesu Kristu ili kwa mapenzi yake nipate kwa Mungu kile ninachomwomba, Amina. Ukishaisali, tuma nakala angalau tisa kwa watu tofauti tofauti,kasha subili utaona maajabu baada ya siku TISA. Baba yetu ni NOVENA. Sala hii ilianzishwa na Mama Thereza wa Calcutta Mwaka 1952 na haijawahi kukatizwa. Tafadhali itume kwa ndugu na marafiki zako. Hii ni NOVENA yenye nguvu. Haikugharimu kusali na tafadhai usiikatize! Isaliukiwa peke yako, na marafiki zako au hata na familia yako. USHUHUDA. Ni kweli, ni NOVENA ya ajabu, niliipata nikaisali kwa siku tisa, mara nilipomaliza nilipata simu kuitwa kwenye usaili, baadaye nilipata kazi ambayo nalipwa mshahara shilingi 1.5 milioni kwa Mwezi – Alta Precision Air. ARUSHA; Masomo ya sekondari yalikuwa yakinipa shida sana, kila nilipo jitahidi kusoma nilikuwa napata alama ambazo haziridhishi. Nilipata nakala ya sala hii nikiwa najiandaa na mitihani yangu ya mwisho (kidato cha sita) nikaisali na kutoa fotokopi na kuituma kwa marafiki zangu kumi, matokeo ya mitihani yalipotoka, kila mtu alishangaa kuona nina daraja la kwanza. P. KEMUNGE, Air Wing Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Somalia alipata sala hii Mwaka 1998, akaidharau na kuichanachana na kuichoma moto. Baada ya miezi sita, wasaidizi wake na Jeshi waliasi, yakatokea machafuko makubwa mjini Mogadishu na Serikali yake ilipinduliwa. Tangu muda ule vita vilianza na hadi leo, Somalia ndiyo Nchi pekee Duniani isiyokuwa na Serikali! BBC, Mogadishu Nilipata sala hii nikaisali huku nikimwomba Mungu anijalie mchumba mwema, Nilipomaliza siku tisa, nilimwota msichana wa ndoto zangu, baadaye alikuja kuwa mchumba wangu! Asiyetaja jina, Moshi. Nilipata sala hii nikiwa nafanya kazi TPC Moshi, nikaitunza kabatini, baadaye ulitokea mzozo na mwajiri wetu, tukafukuzwa kazi. Nilipokumbuka, nikaitafuta nikaipata na kuisali na familia yangu. Wiki iliyofuata nilirudishwa kazini na kupandishwa cheo na kuongezwa mshahara mara dufu. Mushi Eusebio, Kilimanjaro. Natumaini ushuhuda huu umekufanya uamue. Ukisali ukafanikiwa, usikose kutoa ushuhuda wako. Kila utakacho kiomba utakipata mapema kadiri ya idadi ya watu utakao watumia sala hii, ila ni mara baada ya kuisali kwa siku tisa (9) mfululizo, pia yaweza kukukinga na ajali mbaya au balaa iliyokuwa ikupate. • Ukiituma kwa mtu mmoja, ulichokiomba utakipata baada ya Mwaka mmoja (1). • Ukiituma kwa watu watatu, miezi sita (6) • Watu 8, wiki moja. • Watu tisa, siku tano. • Watu 10, siku tatu. • Watu 15, siku 1. • Watu 20, masaa 3. Ni vema ukamjaribu Mungu kwa mema, kuliko kukaa bure, utajikosesha mibaraka ya Bwana!
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright ©| MKATOLIKI KIGANJANI ||CONTACT US 0757195712 ||KILIMANJARO SKY TECHNOLOGIES| |JEMA SOFTWARE DEVELOPER |JEROME MASSAWE||EMMANUEL MALLYA