Translate

Tuesday, 7 August 2018

NOVENA YA MT RITA

NOVENA YA MTAKATIFU RITA|Posted By JEROME MASSAWE.
Image result for novena  ya mtakatifu rita
NOVENA YA MT RITA SIKU YA TATU
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa pumziko, huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu, najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Rita, unayeng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za Kanisa Katoliki, natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu.
Ninakuamini, kwa hamu nangojea, kupata kile nikiombacho {hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita}.
Nifikishie ombi langu kwa Yesu wa msalaba. Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopitia majaribu, kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu.
Kwa sadaka yako ya kishujaa, uliyomtolea Mungu wana wako, ukiomba wasinajisiwe kwa dhambi; uniombee kwa Mungu. Hicho ni kifo dini cha moyo wako. Kwa njia ya mateso uliyochagua yaani kukaa ndani utawani maisha yako; kupitia mateso ambayo Bwana Yesu Kristo aliruhusu yakupate ili utakaswe katika majonzi yako; kwa njia ya majaribu mengi yaliyokupata na sadaka nyingi ulizotoa; uniombee ili nijaliwe kupewa ombi langu ninalongojea kwa hamu.
Baba Yetu (3),
Salamu Maria (3)
Atukuzwe Baba (3).
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.
Kiongozi: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE: Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
©Vijana Jimbo Katoliki Moshi√
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright ©| MKATOLIKI KIGANJANI ||CONTACT US 0757195712 ||KILIMANJARO SKY TECHNOLOGIES| |JEMA SOFTWARE DEVELOPER |JEROME MASSAWE||EMMANUEL MALLYA