SALA YA MTAKATIFU INYASI
Roho ya Kristo initakase,
Mwili wa Kristo uniokoe,
Damu ya Kristo inilevye,
Maji ya ubavu wa Kristo yanioshe,
Mateso ya Kristo nguvu yanizidishie,
Ee Yesu Mwena unisikilize,
Katika madonda yako unifiche,
Usikubali nitengwe nawe,
Na adui mwovu unikinge,
Saa ya kufa kwangu uniite,
Uniamuru nikusogelee,
Sifa zako niimbe pamoja na Watakatifu wako milele na milele,AMINA
0 maoni:
Post a Comment