Ana (kutoka Kiebrania Hannah חַנָּה, yaani "fadhili") anaheshimiwa kama mama wa Bikira Maria na bibi wa Yesu kadiri ya mapokeo ya Ukristo na Uislamu, ingawa hatajwi katika Biblia wala katika Kurani, isipokuwa katika kitabu cha karne ya 2 kinachoitwa Injili ya Yakobo.
Humo anatajwa pia mume wake Yohakimu.
Wote wawili wanaheshimiwa kama watakatifu katika madhehebu mengi ya Ukristo, hasa tarehe 26 Julai.
0 maoni:
Post a Comment